SHARE

NA KYALAA SEHEYE

MWANAMITINDO na mshindi wa pili wa taji la Miss Tanzania mwaka (2006), Jokate Mwegelo, amesema anapenda kujulikana zaidi kwa kazi zake za kijamii kuliko skendo ambazo amekuwa akizushiwa nazo na kumfanya kukosa raha.

“Mimi napenda sana kazi za kijamii, nahitaji kusaidia wanawake wenzangu, hizi skendo zinanikosesha raha, ila ninakabiliana nazo nataka jina langu likue kwa bidhaa au kitu kikubwa ninachoifanyia jamii yangu na hayo ndiyo malengo yangu, ila sina namna ya kukwepa kashfa japokuwa najitahidi kujiweka nazo kando.”

Jokate ni kati ya warembo wanaofanya kazi kubwa kwa jamii akiwa anatamba na lebo yake ya Kidoti ambayo imeanza kutengeneza nywele.

Tayari Jokate ambaye pia ni mwigizaji ameanzisha staili ya nywele na sasa kafumbua kampeni ya msusi wangu ambayo itawapa fursa wasichana wanaojishughulisha na ususi mitaani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here