Home Habari Juma Abdul amkaribisha Kessy Yanga

Juma Abdul amkaribisha Kessy Yanga

513
0
SHARE

kessy alvezNA ZAINAB IDDY

BAADA ya Yanga kumsajili Hassan Ramadhan ‘Kessy’, beki wa kulia wa kikosi hicho, Juma Abdul, amesema kuwa hana shaka na nafasi yake kwenye timu hiyo na badala yake anamkaribisha mwenzake huyo  ili kuongeza changamoto kwenye kikosi chao.

Abdul ameliambia DIMBA kuwa ujio wa Kessy ndani ya kikosi chao utaongeza  ushindani mkubwa kwani kila mmoja anao uwezo na kocha ndiye atakayeamua.

“Sina shaka kabisa na ujio wake, naamini yeye ni mchezaji kama mimi na mpira ni kazi yake, hivyo namkaribisha kwa furaha kwani  naamini  kuna vitu atakuwa navyo ambavyo vitanisaidia mimi pamoja na timu kwa ujumla.

“Naamini Kessy ni mchezaji anayejua nini anafanya uwanjani, hivyo kuja kwake Yanga kutaongeza ushindani wa namba jambo litakaloweza kujituma zaidi kwetu na hivyo kuifanya Yanga kuwa na beki bora zaidi,” alisema Abdul.

Kessy amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili, jambo linaloonekana kutishia nafasi ya Abdul ndani ya kikosi hicho lakini mwenyewe haogopi changamoto hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here