Home Makala Juma Nature kama isingekuwa muziki angecheza Yanga-3

Juma Nature kama isingekuwa muziki angecheza Yanga-3

3295
0
SHARE

NA WINFRIDA MTOI

TAYARI ameshaanza kufahamika kutokana na kufanya vizuri kwa albamu yake inayoitwa ‘Nini chanzo’, maisha ya muziki na soka yanaendelea…endelea kufuatilia..

“Baada ya albamu hiyo kutoka ndiyo watu wakaanza kunijua zaidi kwa sababu awali walikuwa wananijua kupitia nyimbo za kushirikishwa pekee, mimi nilianza kwa kushirikishwa, zipo nyimbo nyingi sana  unaweza kusema za kwangu.

“Kupitia P. Funk Majani, nilitengeneza albamu nne, ya kwanza ni hiyo Nini Chanzo, ya pili Ugali, albamu ya tatu  Ubinadamu Kazi na mwisho ni albamu ya Histori.

Anaeleza kuwa baada ya kumaliza albamu ya nne akiwa chini ya mtayarishaji huyo aliyemfanya jina lake kuwa juu, ndio likaja kundi la TMK Wanaume Family na kujiunga ambako pia alikutana na kina Chege, Temba, Inspekta Haron, Luteni Kalama na wengine.

Akiwa TMK Wanaume walifanikiwa kutoa nyimbo kadhaa, lakini ilitokea hali ya kutoelewana na msimamizi wa kundi hilo, Said Fella, waliamua kuanzisha TMK Wanaume Halisi na ikawepo TMK Wanaume Family.

“Makundi yote mawili tulikuwa tunapiga kazi pamoja kwa ushirikiano kama makundi isipokuwa lile la East Coast na TMK Halisi ambalo lipo hadi sasa ninalisimamia mimi pamoja na wasanii mbalimbali.”

Ushirikina, kipato vyasitisha ndoto yake ya kucheza Yanga

Kabla ya kuingia katika muziki, ndoto kubwa ya Nature ilikuwa ni kucheza soka na timu iliyokuwa inamvutia kuicheza ilikuwa ni Yanga, yenye maskani yake Jangwani, jijini Dar es Salaam.

Nature anaelezea kuwa tangu akiwa na umri mdogo alikuwa akicheza mpira wa miguu katika timu za mitaani na kushiriki ligi mbalimbali ikiwamo Daraja la Tatu.

“Ndoto yangu ya kwanza ilikuwa kucheza soka, awali nilikuwa sina mpango wa kufanya muziki, akili yangu yote kipindi hicho, ilikuwa ni kucheza  timu ya Yanga.

“Katika pita pita katika timu mbalimbali nimecheza na kina Chuji, Boban na Mandate, nilikuwa nacheza sana mechi za ndondo mtaani.

Kipaji cha kucheza soka ninacho na hata safari yangu ya soka haikuishia katika timu au wachezaji wa mitaani kwani nemawahi kucheza pamoja na wachezaji wenye majina kama vile Athumani Idd ‘Chuji’ na Haruna Moshi ‘Boban’ ambao wote wamewahi kuzicheza timu kubwa hapa nchini, Simba na Yanga.

“Lakini kitendo cha kupata majeraha kila mara, ikamfanya baba yangu mzee Kassim kuanza kunikataza  kujihusisha na mchezo huo, alikuwa ananihurumia kuniona naumia mara kwa mara kutokana na umri wangu kuwa mdogo.

Je, baada ya kuachana na soka moja kwa moja alichukuwa hatua gani? Endelea ndani ya Dimba Jumapili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here