SHARE

TURIN, ITALIA

KLABU ya Juventus bado imeendelea kufukuzia saini ya kiungo wa Manchester United, Paul Pogba, huku ikitaka kumalizana naye kabla ya dirisha la usajili nchini Italia halijafungwa mwanzoni mwa mwezi ujao.

Nyota huyo alikuwa akitakiwa na matajiri Real Madrid ambao walishindwa kufika dau la Pauni milioni 180 ambalo linatakiwa na United.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Calciomercato cha nchini Italia, Juve haijaachana na mpango wa kumrejesha nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye amewahi kukipiga katika timu hiyo.

Wote wawili, Pogba na wakala wake Mino Raiola, wameweka wazi kuwa kiungo huyo anataka kuondoka kwa mabingwa mara 20 wa taji la Ligi Kuu ya England.

Hata hivyo Mashetani Wekundu ambao watafungua pazia la Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea leo wameshindwa kufanya usajili wa kiungo mwingine wa kati katika dirisha la usajili lililopita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here