SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MFALME wa R&B, Juma Jux, amefunguka juu ya mahusiano yake na mrembo kutoka kiwanda cha Bongofleva, Vanessa Mdee na kudai kuwa tangu aingie kwenye mahusiano hayo hajawahi kuchepuka.

Jux amefafanua kuwa licha ya changamoto mbalimbali anazokutana nazo, lakini amekuwa mwaminifu na ndiyo sababu ameweza kudumu na mrembo huyo hadi sasa.

“Natambua kuna changamoto nyingi kwenye mahusiano, lakini kikubwa naheshimu sana mapenzi na hadi leo sijawahi kutamani kuwa na mahusiano nje ya haya niliyo nayo, yapo matatizo ninayopitia kama binadamu, lakini nashukuru nimekuwa mwaminifu hadi sasa,” alisema Jux.

Aliongeza kuwa, pamoja na safari waliyopitia na mpenzi wake huyo, lakini wana mikakati mingi ya kuhakikisha wanakuza mahusiano yao na hatimaye kuunda familia kwakuwa ndilo lengo lao kubwa kwa sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here