Home Burudani JUX ANAWEWESEKA KWA VANESSA

JUX ANAWEWESEKA KWA VANESSA

755
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE
MSANII Juma Musa, maarufu Jux, amesema aliyekuwa mpenzi wake, Vanessa Mdee, kwa sasa amekuwa akisingiziwa kuwa na mahusiano na watu wengine kutokana na hali ya uhusiano wao ulivyovunjika.
Jux amesema pamoja na kuridhia kuachana na mwanadada huyo, lakini wamekuwa wakishirikiana katika kazi na ataendelea kumsapoti pale atakapohitaji msaada wa kikazi.
“Leo utaambiwa Vanessa yupo na huyu, kesho yule, lakini yeye ndio mwenye maamuzi ya mwisho katika kuchagua maisha yake, nadhani kuachana kwetu kusiwape watu maneno ya kuongea na badala yake waishi wao na si kufuatilia Jux kafanya nini ama Vanessa kafanya nini,” alisema Jux.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here