Home Habari KAGERE AMNYANYUA KITINI WAZIRI MKUU

KAGERE AMNYANYUA KITINI WAZIRI MKUU

4007
0
SHARE

NA JESCA NANGWAWE

BAO maridadi alilolifunga Meddie Kagere jana dhidi ya JS Saoura, lilimfanya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, kunyanyuka kwenye kiti na kupiga makofi huku akiachia tabasamu la nguvu.

Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 lakini bao la tatu lililofungwa na Kagere ndilo lililoonekana kumkosha zaidi Waziri Mkuu.

Bao hilo lilitokana na pasi nzuri ya Emmanuel Okwi na Kagere kuwazidi mbio walinzi wa wapinzani wao hao na alipomkaribia kipa aliunyanyua mpira na kujaa wavuni ndipo uzalendo ukamshinda Waziri Mkuu na kuamua kunyanyuka akishangilia.

Mbali na Waziri huyo, wengine ambao walionekana kukoshwa na mabao hayo ya Simba ni aliyekuwa mgeni rasmi, Naibu Spika, Tulia Ackson pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe.

Viongozi hao wa Serikali waliungana na bilionea wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, kufurahia kandanda safi lililokuwa likichezwa na vijana wa Simba likinakishiwa na pasi za maana zilizokuwa zikipigwa na viungo kama Clatous Chama, Jonas Mkude pamoja na Hassan Dilunga.

Baada ya ushindi huo sasa Simba wanajiandaa kwenda DR Congo kuwakabili AS Vita Januari 19, mwaka huu kabla ya kwenda kumalizia mzunguko wa kwanza watakapowakabili Al Ahly Februari 1, mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here