SHARE

NA SAADA SALIM

STRAIKA kipenzi cha Wanasimba, Meddy Kagere, beki Erasto Nyoni na Haruna Niyonzima, leo watasafiri kwenda kuungana na wachezaji wenzao kambini nchini Uturuki, huku wakitoa maneno ya faraja kwa mashabiki.

Wakati wakijiandaa na safari hiyo, Kagere aliliambia DIMBA Jumatano kwamba, katu hahofii kupata namba katika kikosi cha Wanamsimbazi kwani anaamini amekuja nchini kufanya kazi.

“Unajua hakuna sehemu ambayo utakwenda na ukakosa ushindani, nafurahi kukutana na washambuliaji ambao sikucheza nao Kombe la Kagame, nina imani tunaenda kutengeneza ushirikiano na kujenga uimara wa safu ya ushambuliaji,” alisema.

Kagere alisema licha ya kikosi hicho kusheheni washambuliaji wenye uwezo mkubwa, lakini atapambana kuhakikisha anapata namba.

Safu hiyo ya ushambuliaji ya Simba msimu huu inaonyesha itakuwa na vita kali kutokana na uwepo wa Emmanuel Okwi, John Bocco, Kagere, Adam Salamba, Moses Kitandu pamoja na Mohamed Rashid ‘Mo Rashid’.

Kwa sasa kikosi hicho kipo nchini Uturuki na akina Kagere wakitarajiwa kuungana na wenzao na kuendelea kujifua

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here