Home Habari KAMUSOKO AFICHWA HADI MECHI YA MBAO

KAMUSOKO AFICHWA HADI MECHI YA MBAO

3251
0
SHARE

NA SAADA SALIM

YANGA wajanja sana, kwani wameona wakimtumia kiungo wao, Thaban Kamusoko mapema wanaweza wakaendelea kutonesha majeraha yake, ndipo wakaamua kumpumzisha mchezo wa jana na sasa anasubiri mchezo ujao dhidi ya Mbao FC.

Kiungo huyo amelazimika kukosa baadhi ya michezo kutokana na majeraha yanayomkabili na sasa atasubiri mpaka michuano ya Chalenji, itakayofanyika kuanzia Desemba 3, mwaka huu, nchini Kenya imalizike, ndipo arejee uwanjani, na mchezo atakaoukuta ni dhidi ya Mbao FC.

Akizungumza na DIMBA jijini Dar es Salaam, daktari anayemtibu mchezaji huyo, Nassor Matuzya, alisema matibabu yamekwenda vizuri na anatarajiwa kuanza kujifua wiki ijayo, ili kujiweka vizuri kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mbao FC.

“Kuanzia wiki ijayo Kamusoko anatakiwa kuanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kuweka mwili wake fiti, kabla ya kuungana na wenzake, naamini mpaka michuano ya Chalenji inamalizika, atakuwa amepona vizuri,” alisema.

Kamusoko amekuwa tegemeo kubwa ndani ya klabu hiyo kutokana na aina ya uchezaji wake wa kujituma, ndiyo maana anapopata majeraha yanayomuweka nje ya uwanja, mashabiki wake huwa na wasiwasi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here