LAS VEGAS, Marekani
MWANAMUZIKI Chance the Rapper amemkingia kifua mwenzake wa Hip hop, Kanye West, akisema uamuzi wake wa kuimba ‘gospo’ hautokani na tamaa ya fedha kama inavyoelezwa.
Kanye aliachia albamu yake ya kwanza ya muziki wa Injili, Jesus is King, ambayo imewagawa mashabiki na wadau wa muziki, baadhi wakisema amefuata mkwanja.
Akilizungumzia hiyo, Chance the Rapper alisema Kanye ni mfano mzuri wa namna wasanii wa Kikiristo wanavyopaswa kutumia sauti zao kumwimbia Bwana.