SHARE
LOS ANGELES, CA - OCTOBER 25: Kourtney Kardashian attends the PrettyLittleThing By Kourtney Kardashian Launch on October 25, 2017 in Los Angeles, California. (Photo by JB Lacroix/ WireImage)

LOS ANGELES, Marekani

MWANAMITINDO, Kourtney Kardashian, amesema yuko tayari kuishi peke yake tena na hana mpango wa kuingia katika mahusiano na mtu mwingine hata mzazi mwenzake, Scott Disick.

Taarifa zilizoripotiwa na TMZ ni kwamba Kardashian aligawana vitu na aliyekuwa mchumba wake mwenye miaka 25, Younes Bendjima, ambaye alinaswa na kamera akiwa na mrembo mwingine nchini Mexico.

Katika sherehe ya kuzaliwa ya Kylie ambaye alikuwa akitimiza miaka 21, Kourtney alionekana akiwa bega kwa bega na mzazi mwenzake, Disick.

Nyota huyo wa kipindi cha Keeping up with the Kardashian, alisema kuonekana na Scott ni marafiki hakuna kinachoendelea baina yao, kwani hivi sasa mzazi mwenzake huyo yuko kwenye mahusiano na mtoto wa gwiji wa muziki nchini Marekani, Sofia Richie, mwenye miaka 19.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here