Home Habari Kaseke apewa jukumu la kuwamaliza Mo Bejaia

Kaseke apewa jukumu la kuwamaliza Mo Bejaia

726
0
SHARE
Deus Kaseke

NA MARTIN MAZUGWA,

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke, amepewa darasa  la kuwamaliza Mo Bejaia mara baada ya kukosekana katika mchezo wa marudiano ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Medeama.

Mchezaji huyo ambaye amekuwa muhimu kutokana na kasi yake uwanjani akiwa fundi wa kuanzisha mashambulizi na kuzuia, alikosekana katika mchezo dhidi ya Medeama kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimkabili.

Katika mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam, kocha Hans Pluijm alionekana akitengeneza mfumo utakaompa nafasi ya kucheza kwenye mchezo huo dhidi ya Mo Bejaia.

Kwa upande wake kocha msaidizi wa timu hiyo, Juma Mwambusi, naye alionekana akimpa maelekezo mchezaji huyo ambaye alitoka naye katika kikosi cha wagonga nyundo wa Jiji la Mbeya, Mbeya City.

Kurudi uwanjani  kwa kiungo huyo mshambuliaji katika kikosi cha kwanza cha vijana wa  Jangwani kutakuwa na faida kubwa  kutokana na uwezo na  ubora wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here