Home Habari Didier Kavumbagu: Simba njooni mezani

Didier Kavumbagu: Simba njooni mezani

882
0
SHARE

kavuNA SAADA SALIM

STRAIKA wa kimataifa wa Azam FC Mrundi, Didier Kavumbagu, amesema yupo tayari kusaini mkataba na kuichezea Simba msimu ujao kama viongozi wa klabu hiyo watakaa naye mezani.

Akizungumza na DIMBA jana, straika huyo alisema kutokana na mkataba wake na Azam FC upo ukingoni pia hakuna kiongozi yeyote aliyewasiliana naye kwa ajili ya kuongeza mkataba hivyo yuko tayari kusaini Simba kama watahitaji huduma yake.

Alisema kama mchezaji anachokiangalia zaidi ni masilahi na kama Simba wanamfuata na kutaja dau atakalokubaliana nalo atasaini na kucheza Simba.

“Muda wowote kuanzia sasa mkataba wangu na Azam FC unafikia mwishoni, hivyo Simba wakiwa tayari na dau lao zuri basi nitasaini na kuchezea Simba sina tatizo la jambo hilo,” alisema.

Kavumbagu alisema pia amefanya mazungumzo na uongozi wa Mbeya City kwa ajili ya kusaini lakini amewapa masharti kama watayatekeleza na Simba hawajaeleweka ataweza pia kucheza Mbeya.

Kavumbagu mkataba wake upo ukingoni ambapo kwa sasa yupo nchini Burundi kwa ajili ya mapumziko na anatarajia kurejea  nchini Juni 30 mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza hatima yake kuhusu mkataba mpya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here