SHARE

NEW YORK, Marekani

RAPA Kendrick Lamar amefanikiwa kupata mtoto wake wa kwanza mwezi huu baada ya kuficha siri katika kipindi chote cha ujauzito wa mchumba wake, Whitne Alford.

Mkali huyo alimkaribisha duniani mtoto huyo wa kike aliyempata pamoja na Whitney, ambaye alikutana naye miaka 10 iliyopita na licha ya tabia yake ya kuficha masuala yake binafsi, aliamua kuweka wazi kila kitu Aprili 2015.


“Sikuweza hata kumwita ni mwanamke wangu. Nilimuona kama rafiki mwema zaidi kwangu. Kiufupi ni mtu ambaye nina uwezo wa kumwelezea hofu zangu na akanielewa,” alisema Kendrick.


Miezi saba baadaye, mshindi huyo wa tuzo ya Grammy alithibitisha kuwa yeye na Whitney waliingia kwenye uchumba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here