SHARE

 

NA ZAITUNI KIBWANA

UNAWEZA kudhani beki kisiki, Ramadhani Hassan ‘Kessy’ ameibuka kwenye mazoezi ya Simba yanayoendelea katika kambi iliyopo ndani ya kituo cha Highland mjini Morogoro, baada ya jezi yenye jina lake kutumiwa katika mazoezi hayo.

Jezi hiyo namba 4 aliyokuwa akiivaa mchezaji huyo ambaye kwa sasa amehamia Yanga huku akisikilizia huruma ya Simba ili aweze kukipiga katika timu yake hiyo mpya, ilileta mshangao kwa washabiki wachache walioruhusiwa kuona mazoezi hayo, wakidhani aliyevaa jezi hiyo iliyoandikwa pia jina la Kessy ndiye mchezaji mwenyewe.

Hata hivyo, DIMBA lilimshuhudia Kessy mwenyewe akiendelea na mazoezi na timu yake ya Yanga yaliyokuwa yakifanyika jana kwenye Uwanja wa Boko Veterani uliopo Boko, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Mmoja wa viongozi aliyekuwepo kwenye mazoezi ya Simba alilidokeza gazeti hili kuwa wamelazimika kutumia jezi za wachezaji mbalimbali hata walioachwa kwa vile bado wanazo nyingi na nyingine bado mpya kabisa na hazijawahi kutumiwa.

Simba imeweka kambi mkoani Morogoro ili kumpa nafasi kocha mpya wa timu hiyo raia wa Cameroon, Joseph Omog, kuwafanyia tathmini wachezaji atakaowasajili kwa ajili ya kuichezea timu hiyo msimu ujao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here