SHARE

ABDULAH MKEYENGE


UNAIKUMBUKA ile mechi ya Ngao ya Jamii mwaka huu iliyopigwa katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kwa Simba kushinda bao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar na kutwaa ubingwa huo kwa mara mbili mfululizo.
Mbali na ushindi huo wa Simba, lakini walifungwa bao moja matata nje ya boksi na Kelvin Sabato ‘Kongwe’ ambaye alipiga shuti kali na kumwacha kipa bora wa nchi, Aishi Manula, kuuokota mpira huo nyavuni.
Moto huo ambao alionesha Kongwe, ametamba kufanya hivyo hata katika mechi za ligi na hata katika timu ya Taifa ambayo ameitwa kwa mara ya pili.
Akizungumza na DIMBA, Kongwe aliyeitwa katika kikosi cha Taifa Stars ya kocha Mnaigeria Emmanuel Amunike, ambacho kitaivaa Uganda Novemba 8, ametamba kuendeleza moto wake wa kufunga mabao.
“Katika nafasi yangu, kuna wachezaji wakubwa ambao ni wanachama soka nje ya nchi, lakini kama atapata nafasi ya kucheza atafanya kile ambacho benchi la ufundi linataka kutoka kwake,” alisema Kongwe.
Kikosi cha Stars kina washambuliaji wanne wanaocheza soka la kulipwa nje ya mipaka ya Tanzania ambao ni Mbwana Samatta, Farid Mussa, Shaban Iddy ‘Chilunda’ na Thomas Ulimwengu.
Katika hatua nyingine, Kongwe anasema hadi sasa ameitwa katika kikosi cha Stars kuna kitu cha ziada ambacho ameonyesha katika ligi na kumshawishi kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Emmanuel Amuneke.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here