Home Habari Kichuya, Mobby waingia rada za Simba

Kichuya, Mobby waingia rada za Simba

501
0
SHARE

SHIZZA KICHUYANA SAADA SALIM

KUMEKUCHA! Hii ni baada ya uongozi wa Simba kupeleka majina ya wachezaji wawili, Shiza Kichuya na Iddy Mobby, katika kamati ya usajili ili kujadiliwa na kama wakikubaliwa wasajiliwe kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba ambao wako katika mchakato huo wa kuangalia wachezaji watakaoitumikia msimu ujao, imeamua kutafuta saini ya wachezaji hao ili kuweza kuongezea nguvu katika kikosi chao huku Kichuya anayetokea Mtibwa Sugar na Mobby wa Mwadui FC wakiwa ni wachezaji wa kwanza kumulikwa.

Taarifa za uhakika zilizolifikia DIMBA kutoka ndani ya kamati hiyo ya usajili iliyopo chini ya mwenyekiti wake, Zacharia Hanspope, tayari majina ya wachezaji hao yameshatua mezani kwao kwa ajili ya utekelezaji.

“Kwa sasa kamati ipo makini katika usajili, imeanza na wachezaji hao kupelekwa katika kamati hiyo ya usajili kwa kujadiliwa na kuna uwezekano mkubwa wa kufanya nao mazungumzo.

“Unajua Mobby ni beki mzuri sana, staili anayocheza haina tofauti kabisa na anavyocheza Kelvin Yondani, ukiangalia katika mechi ya Mwadui na Yanga alifanya kazi kubwa ikimaanisha kwamba ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kuwa msaada mkubwa katika kikosi cha Simba.

“Kwa upande wa Shiza yeye hakuna sababu ya kumwelezea sana ila ameonekana ni moja ya wachezaji bora katika ligi yetu ya Tanzania  Bara, uongozi umeona kwamba anaweza kusaidiana na wale waliopo kikosini kwa sasa ili kuiletea Simba mafanikio,” kilisema chanzo chetu kilichopo karibu na kamati ya usajili ya Simba.

Shiza ni miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri kwenye mechi za Kombe la Mapinduzi mwaka huu, lakini hata kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara huku Mobby akitajwa kuwa miongoni mwa mabeki bora katika ligi ya msimu huu akiwa na kikosi cha Mwadui FC kinachonolewa na Kocha Jamhuri Kihwelu ‘Julio’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here