Home Habari Kichuya: Mtamsahau Okwi Simba

Kichuya: Mtamsahau Okwi Simba

1197
0
SHARE

NA ZAINAB IDDY

KIUNGO mpya wa Simba, Shiza Kichuya, ametamka wazi kuwa umefika wakati wa Wanamsimbazi kumsahau straika  wa kimataifa wa Uganda, Emannuel Okwi, kwani anaweza kuvaa viatu vyake.

Moja ya mambo ambayo tayari Kichuya amemrithi Okwi ni kuchukua jezi yake namba 25 ambayo aliivaa katika mchezo dhidi ya AFC Leopard ya Kenya kwenye tamasha la ‘Simba Day’ mchezo uliomalizika kwa ushindi wa mabao 4-0.

Lingine ambalo winga huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amefanikiwa kulifanya kwa muda mfupi ni kiwango kizuri anachokionyesha na hilo lilijidhihirisha kwenye mchezo huo dhidi ya Wakenya hao.

Kichuya ameliambia DIMBA Jumatano kuwa ataitendea haki jezi hiyo namba 25 ambayo ilikuwa inavaliwa na Okwi na kwamba atawasahaulisha yote ya nyuma.

“Nimevaa jezi hii nikiwa siogopi kuzomewa, kupigwa na chupa wala kuzungumzwa vibaya na mashabiki pale nitakapokuwa natimiza majukumu yangu ipasavyo, hivyo jezi namba 25 ipo akilini mwangu ili niilindie heshima yake.

“Kama Okwi atasajiliwa na Simba msimu ujao na akaitaka jezi yake nitampatia ila nataka kwanza niitendee haki ipasavyo ili nikiikabidhi kila mmoja aridhike kwamba ilikuwa kwenye mikono salama,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here