Home Burudani Kifo cha Ruge chakatisha ndoto za Sam Sukari

Kifo cha Ruge chakatisha ndoto za Sam Sukari

1583
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU

KIFO cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, kimemvuruga msanii anayekuja juu katika muziki wa kizazi kipya, Sam Sukari, kwa kuwa aliahidiwa makubwa na mlezi wa wasanii wengi wakubwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Sam Sukari ambaye ni zao la kampuni ya Nyumbani Studios inayomsimamia, alisema alikutana na marehemu Ruge wakati wa uhai wake na alipomwelezea kuhusu harakati zake za kimuziki, aliahidi kumsaidia endapo tu atajitahidi kutambaa na yeye atamsaidia kusimama.

“Nilikutana na Ruge na niliongea naye juu ya vipi anaweza kunisaidia kimuziki, aliniambia anaweza lakini nijitahidi kutambaa kwanza mimi mwenyewe, yeye yupo tayari kunishika mkono ili nisimame, akaniambia niwe naye karibu kimawasiliano kwa sababu yeye ni mlezi wa wasanii wengi hivyo ana mambo mengi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here