Home Habari Kikosi cha wachezaji 17 wa Simba SC charejea Dar kuwakabili Waarabu

Kikosi cha wachezaji 17 wa Simba SC charejea Dar kuwakabili Waarabu

3599
0
SHARE

SAADA SALIM NA LULU RINGO

Kikosi cha Wachezaji 17 wa Simba SC waliokuwa wakishiriki Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar wamerejea Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi yao ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya JS Saoura itakayopigwa Uwanja wa Taifa Jumamosi ya Januari 12.

Baadhi ya wachezaji hao wamerejea huku wakiwa wameshaisaidia timu hiyo kuingia nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayoendelea kufanyika visiwani humo.

Wachezaji waliorejea ni Pascal Wawa, Deogratius Munishi (Dida), Clatous Chama, Mzamiru Yasin, Aish Manula, Meddie kagere, James kotei na Mohamed Hussein (Tshabalala).

Wengine ni Nicholas Gyan, John Bocco, Haruna Niyozima, Jonas Mkude, Emmanuel Okwi, Ramadhani kichuya, Said Hamis (Ndemla), Rashid Juma na Hasan Dilunga.

Wachezaji waliobaki ni Ally Salim, Paul Bukaba, Asante Kwasi, Yusuph Mlipili, Adam Salamba, Abdul Selemani na Zana Coullibaly ambao wataungana na timu B ya Simba iliyotua leo Januari 9 visiwani humo kwenye mchezo wa nusu fainali.

Simba SC imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo jana Januari 8 baada ya kuichapa Mlandege ya Zanzibar bao 1-0, bao lililofungwa dakika ya 20 na kiungo Mnyaruwanda Haruna Niyonzima kwa mkwaju wa penati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here