SHARE

BOLOGNA, Italia

KINDA wa Nigeria ambaye pia anakipiga katika kikosi cha vijana cha taifa hilo, Orji Okoronkwo, amesema dhamira yake ya kucheza kwenye Ligi ya Italia ni kupata nafasi zaidi kimataifa na kwamba anachokitafuta yeye ni mafanikio.

Nyota huyo amesisitiza kwamba, uwezo wa kucheza ligi ya Italia umeonekana, lakini suala la kulinda uwezo huo na kuweza kufanikiwa katika mipango yake ni jambo lingine kubwa zaidi.

“Wapo vijana wengi wanaopata nafasi kama hizi lakini hawajafanikiwa kwa sababu tofauti tofauti, lakini niseme kwamba mimi sina tatizo na hilo, kwa sababu natafuta mafanikio kuliko kupata sifa.

“Nina imani kwamba kama mambo yatakwenda vizuri, ninaweza kuwa mmoja wa wachezaji wakubwa duniani kwa sababu hapa Italia ni mahali sahihi, ila juhudi na maarifa zaidi yanahitajika,” alisema Okoronkwo, ambaye anakipiga katika kikosi cha Bologna.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here