SHARE
Gianluigi Donnarumma

MILAN, Italia 

MKURUGENZI wa michezo katika klabu ya PSG, Leonardo, anammezea mate kipa wa AC Milan, Gianluigi Donnarumma, lakini anapata presha kutoka kwa kocha mkuu wa Chelsea, Frank Lampard. 

Japo klabu zote mbili zimeonyesha nia ya kumnasa nyota huyo wa Milan, lakini wote pia wanapendekeza liwe dili la kubadilishana wachezaji. 

Leonardo anafikiria kuongeza Alphonse Areola kwenye mazungumzo wakati Lampard naye anafikiria vivyo hivyo na kutaka kumtoa Kepa Arrizabalaga katika dili lolote.

Hata hivyo kwa mujibu wa gazeti la Tuttosport, Rossoneri wao wanataka kumuuza moja kwa moja Donnarumma na kupata fedha.

Hii inamaanisha AC Milan wataitisha kitita kikubwa ambayo inaweza ikawakimbiza Chelsea lakini PSG haitawasumbua sana kwa sababu wanaamini wanawez kupata fedha nyingi kama watamuuza Neymar kurudi Barcelona. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here