SHARE

NA TIMA SIKILO

KIPA wa timu ya KMC, Jonathan Nahimana,amesema kwa sasa yupo nchini Burundi kwa mapumziko lakini pamoja na hilo anaitumia fursa hiyo kuangalia majembe mapya anayoweza kuiletea timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
Akizungumza na DIMBA,alisema,Nahimana alisema,alisema,Burundi imejaaliwa wachezaji wengi wenye vipaji vya ambao anaamini wanaweza kuipa mafanikio makubwa KMC.
Alisema, yeye ana mpango wa kuleta wachezaji wawili kutoka nchini huko mara Ligi itakaporuhusiwa kuendelea.
“Wachezaji wazuri ni wengi ila mimi nitakuja na wachezaji wawili mshambuliaji na beki naamini hapo hakuna atakayekosa timu ya kucheza nchini Tanzania kwani wana viwango vizuri, ” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here