Home Michezo Kimataifa KIPA MAREKANI ASHINDWA KUVUMILIA MAOVU YA BLATTER

KIPA MAREKANI ASHINDWA KUVUMILIA MAOVU YA BLATTER

562
0
SHARE

NEW YORK, Marekani

MLINDA mlango wa timu ya Taifa ya wanawake Marekani, Hope Solo, amefichua kitendo cha udhalilishaji alichofanyiwa na rais wa zamani wa Fifa, Sepp Blatter, kwa kugusa makalio yake mwaka 2013 kwenye hafla ya tuzo za mchezaji bora wa mwaka.

Solo, alizawadiwa tuzo ya mchezaji bora wa kike wa mwaka katika hafla hizo na alidai kuwa Blatter alimgusa makalio bila ridhaa yake.

“Sepp Blatter alinishika makalio,” alisema Solo.

Solo alifunguka zaidi na kutaja sababu kwanini hakulisema hilo tangu awali na hajamfuata Blatter kuzungumza naye.

“Nilikuwa nina hofu wakati wa kuzungumza na baada ya kile kitendo sikumfuata na kumwambia wazi ‘usinishike tena’. Niliamua tu kukaa nalo moyoni,” alisema Solo alipokuwa akihojiwa na mtandao wa Tribuna Expresso.

Mtandao huo pamoja na gazeti la The Guardian, walimtafuta msemaji wa Blatter ambaye alisema madai hayo ya Solo ni ‘ya kushangaza’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here