Home Habari KIPA SIMBA KURUDI JUMAMOSI NA SALMA MPELI

KIPA SIMBA KURUDI JUMAMOSI NA SALMA MPELI

1223
0
SHARE

KIPA SIMBA KURUDI JUMAMOSI

NA SALMA MPELI

KIPA wa Simba, Said Mohamed ‘Nduda’, anatarajiwa kurudi nchini Jumamosi ya wiki hii akitokea India alipokwenda kufanyiwa upasuaji wa goti.

Akizungumza na DIMBA jana kwa mtandao kutoka India, Nduda alisema anashukuru Mungu anaendelea vizuri tangu afanyiwe upasuaji na amesharuhusiwa kutoka hospitalini lakini kesho anatarajia kuonana tena na daktari wake.

Alisema atakwenda kumwona daktari huyo kwa ajili ya kumfanyia vipimo vya mwisho na kuangalia maendeleo yake kabla ya kumruhusu kurudi.

Alipoulizwa kuhusu muda atakaokaa nje ya uwanja, Nduda alisema kuwa bado hajaambiwa kuhusu hilo lakini kesho atakapokutana na daktari wake huyo ndipo atakapojua.

Nduda aliumia goti mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu akiwa na kikosi cha Simba kilipokuwa kambini visiwani Zanzibar wakijiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.

Kutokana na majeraha hayo, kipa huyo aliyesajiliwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar, alilazimika kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili na zaidi kabla ya kwenda India kufanyiwa matibabu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here