SHARE

NA JESSCA NANGAWE

UONGOZI wa klabu ya Simba jana ulifanya kikao cha ghafla kujadili mambo mbalimbali kubwa ikiwa ni kuwalinda nyota wake na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona.

Kupitia kikao hicho kwa kauli moja wajumbe walikubaliana kwamba nyota wote wa kigeni waliokwenda likizo watakaporudi watengewe karantini maalumu ili kuwalinda wachezaji wengine na hatari ya virusi vya ugonjwa huo unaotikisa dunia.

Miongoni mwa nyota waliotimkia makwao likizo ni pamoja na Meddie Kagere, Luis Miquissone, Clatous Chama na Sharaf Shiboub.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, alisema,mjadala mkubwa kwenye kikao hicho ulikuwa janga la corona ambapo wachezaji wa kigeni walioondoa nchini wanapaswa kurejea na kukaa karantini kwa uchunguzi zaidi kabla ya kuingia kambini.

Alisema, walikubaliana kwamba wanapaswa kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu kuhusu ugonjwa huo kama sehemu ya kuwalinda nyota wake na jamii kwa ujumla.

Ni kikao kilichokua kinahusu maendeleo ya timu yetu lakini kubwa pia ni elimu ya jinsi wachezaji wetu wanapaswa kukaa kipindi hiki dunia inapambana na ugonjwa wa Coronaîalisema Rweyemamu.

Aidha kwa mujibu wa daktari wa timu hiyo Yassin Gembe,wameandaa mazingira ya kuwaweka wachezaji kambini ikiwemo kutumia vifaa vyote ambavyo vinavyohitajika kipindi hiki maambuziki yanaendelea kusambaa.
Simba ambao ni mabingwa watetezi wameendelea kuongoza Ligi hiyo wakiwa na alama 71 mpaka sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here