SHARE

NA JESSCA NANGAWE

STAA kutoka kiwanda cha Bongomovie Wema Sepetu amefunguka kuwa hataki atambulike kama mwanamke wa zamani wa Diamond kwa kuwa ana nafasi nyingi zinazomtambulisha.

Wema ambaye mara nyingi kwenye mahojiano amekua akitambulishwa kama mpenzi wa Diamond amesema hataki tena kusikia hivyo na badala yake watu watumie nafasi zake nyingine kumtambulisha.

‘Haya mambo yameshapitwa na wakati,mbona kuna nafasi nyingi ninazo..mf.miss Tanzania aliyepita na mengine..naomba hilo life,’alisema Wema.

Wema aliongeza amekua akipambana kutengeneza jina lake kwa maana nyingi lakini kubwa kuzidi kujiweka kwenye nafasi ya kutambulika zaidi na si kutumia majina ya watu kumtambulisha.

Kauli ya Wema imekuja baada ya kuhojiwa na kituo cha redio nchini Kenya huku kikimtambulisha kama mpenzi wa zamani wa Diamond na kuamua kutoa ya moyoni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here