SHARE

TURIN, Italia

JUVENTUS wanafikiria kumtoa Federico Bernardeschi kama sehemu ya mabadilishano ya kumpa kiungo wa Barcelona, Ivan Rakitic ambaye tangu kuanza kwa msimu huu amekuwa hatapi nafasi ya kuanza mara kwa mara kwa Wacatalunya hao.

Mabingwa hao wa Italia wanaamini Bernardeschi ni mchezaji sahihi ambaye atawafaa Barcelona huku ikidaiwa kama usajili huo utakuwa mgumu, basi wataongeza na kitita cha pauni milioni 10 ili kuwavutia wakali hao wa Hispania.

Itakumbukwa wapinzani wa Juventus katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Italia, Inter Milan walikuwa wanavutiwa na mpango wa kumsajili kiungo huyo raia wa Croatia lakini waligonga mwamba kwenye dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Pia, imebainika Rakitic amekuwa akisukuma uhamisho wake ndani ya Barcelona, waliopo karibu wanasema mchezaji huyo havutiwi tena na mpango wa kuendelea kuwepo Camp Nou.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here