Home Michezo Kimataifa KIUNGO LIVERPOOL NJE MIEZI KADHAA

KIUNGO LIVERPOOL NJE MIEZI KADHAA

616
0
SHARE

LIVERPOOL, England

KIUNGO wa Liverpool, Adam Lallana, atakosa ‘miezi kadhaa’ ya msimu mpya wa Ligi Kuu England baada ya kupata majeraha ya paja, kocha wa timu hiyo, Jurgen Klopp, amethibitisha.

Lallana, mwenye umri wa miaka 29, aliumia wakati akiitumikia timu yake katika mchezo wa fainali wa Kombe la Audi, ambapo walipoteza kwa Atletico Madrid Jumatano iliyopita.

“Nadhani tunaweza kumwondoa kucheza Agosti na Septemba, na hii siyo habari ambayo tulitaka,” alisema Klopp.

Majeraha hayo yatamfanya Lallana, ambaye ameichezea timu yake ya taifa ya England, kukosa michezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwezi ujao dhidi ya Malta na Slovakia.

Liverpool ilipoteza mchezo wake wa kwanza kuelekea msimu mpya wa ligi baada ya kufungwa kwa penati 5-4 dhidi ya Atletico Madrid, jijini Munich, Ujerumani, baada ya timu zote mbili kutoka sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here