SHARE

LIVERPOOL, ENGLAND

MARA baada ya nyota wawili wa klabu ya Liverpool, Roberto Firmino na Allisson Beker,  kupata bahati kwa mara ya pili baada ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa na kufanikiwa kulisaidia taifa lao kubeba kombe la Copa America jambo hilo limefanya kocha wao Jurgen Klop ashindwe kuficha hisia zake na kuwapongeza vijana wake.

 “Niliwaandikia ujumbe wote wawili mara baada ya mchezo.

 “Nimewatumia video nyingi , ujumbe wa sauti na vitu vingine kama hivyo , walikuwa na wakati mzuri na jumbe ya mwisho nimepata, hakika wanahitaji mapumziko wana haki hiyo.

“Ni vizuri tena vizuri sana kuwaona wakishangilia tena nilipoangalia picha  mara baada ya mchezo Brazili walipokuwa wakisherehekea walinikumbusha wiki tano zilizopita,” alisema Klop.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here