Home Habari Kocha Leopards aondoka na Mavugo

Kocha Leopards aondoka na Mavugo

0
SHARE

NA SAADA SALIM

KOCHA Mkuu wa AFC Leopards ya Kenya, Ivan Minndert, amemvulia kofia straika wa Simba Mrundi, Laudit Mavugo, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kwenye mchezo wa ‘Simba Day’ mwanzoni mwa wiki hii.

Mbali na Mavugo, pia kocha huyo amemtaja winga Shiza Kichuya na straika Ibrahim Ajib kwamba wana viwango vya hali ya juu na kama wakitumika vizuri watafika mbali.

Katika mchezo huo wa maadhimisho ya miaka 80 ya Simba, Wekundu hao wa Msimbazi waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 yakifungwa na Kichuya, Mavugo na Ajib aliyefunga mawili.

Akizungumza baada ya mchezo huo kocha huyo alisema Simba walicheza vizuri kila idara huku akiwamwagia sifa kemkem wachezaji hao watatu na kuutaka uongozi wa Simba kuwalea vizuri kwani watakuja kuona matunda yao baadaye.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here