SHARE

NA MWAMVITA MTANDA

KOCHA Mpya wa Yanga, Luc Eymael ametumia saa mbili ya  kuhoji wachezaje wake kila mmoja ili kujua tatizo lake kabla ya kujua jinsi ya kumpa nafasi katika kikosi chake.

Eymael ameanza  mazoezi ya kwanza na kikosi Jumapili wiki wiki iliyopita, ikiwa ni siku ya nne hadi na tayari ameshatambua uwezo na mapungufu ya kila mchezaji.

Baada ya kumaliza hatua hiyo, Mbelgiji huyo ametenga siku kumi za kufanya mazoezi ya kasi ili kuwasaidia wachezaji kuwa na pumzi na kasi wanapokuwa uwanjani.

DIMBA Jumatano limepata nafasi ya kufanya mahojiano  ya ana kwa ana ili kutambua mpango wake mzima ndani ya kikosi cha Yanga.

ATAKA USAJILI WA MAJEMBE MAWILI

Eymail alisema, wachezaji aliowakuta ndani ya timu ni wazuri na hata ambao wamesajiliwa kati kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo nao ni bora, lakini ameomba viongozi wamuongweze majembe mawili katika nafasi ya Winga na Kiungo.

“Kwa muda wa siku tatu ambazo nimefanya nao mazoezi  nimewasoma vizuri, kwa jumla kila mmoja yuko fiti kwa nafasi yake lakini nahitaji kikosi kipana zaidi ndio maana nimeomba kuongezewa hao wawili kama muda utaruhusu na nafasi kwa viongozi,”alisema Eymael.

AIBUA UDHAIFU WA  ZAHERA

Hata hivyo kocha huyo alisema, mapungufu yaliyopo kwa wachezaji kwa asilimia kubwa yamesababishwa na  aliyekuwa kocha Mkuu wa timu hiyo, raia wa DR Congo, Mwinyi Zahera, hivyo atakuwa nakazi kubwa ya kuwaweka sawa.

Alisema  hana shaka na Charles Boniface Mkwasa, ‘Master’ ambaye  alikuwa anakaimu nafasi hiyo kutokana na wasifu wake, pia ni kama baba ambaye anapenda kuona vijana wake wanafanya vizuri, lakini kocha aliyekaa nao muda mrefu naona alishindwa kuwaimarisha kwa mazoezi ili kuwapa pumzi wachezaji.

“Kwa sasa siwezi kusema mengi bali nahitaji kufanya kazi amabayo imenileta Yanga, lakini inaonekana  mwalimu aliyepita hakuweka mazingira mazuri kwa wachezaji, pengine hiyo hali ndio iliwafanya wengi wao wakate tamaa na kutoona umuhimu wa mazoezi,”alisema Mbelgiji huyo.

ATAKA WACHEZAJI WAHAME HOTELINI

ILI Kuhakikisha mipango yake ya kuimarisha timu inakuwa thabiti, Eymael ameshauri wachezaji wake wote ambao wanakaa Hotelini watafutiwe nyumba za kuishi akidai kuwa hotelini sio mazingira sahihi ya kuishi mchezaji.

“Nina uzoefu mkubwa katika  soka, natambua madhara ya wachezaji ambao wanaishi hotelini kwa muda mrefu, wanakuwa hawapo sawa kisaikolijia kwa kuwa  ile ni kambi hivyo wanakosa kufanya mambo yao binfasi.

“Kwa upande wangu huwa napenda wachezaji wakae kambini siku moja au mbili kabla ya mechi, lakini muda wote wawe wanatokea katika makazi yao,”aliongeza Mbelgji huyo.

AZUNGUMZIA MLO MAALUMU KWA WACHEZAJI

Kuhusu suala la mlo kocha huyo ameshauri chakula maalum kulingana na mahitaji ya wachezaji, tayari ameshaanza kuwapa ratiba  ya kila mmoja kulinga na uzito wake.

Alisema, amewashauri watumie vyakula kwa mpangilio na sio kila kitu wanaweza kula kwa ajili ya kulinda afya zao kwa ajumla.

“ Mchezaji anaruhusiwa kula lakini sio kula kila  anachokiona, anaweza kuumwa tumbo akiwa na anakabiliwa na mechi mbele yake, katika hili nimewaomba wazingatie sana,”alisema Eymael.

KOCHA WA VIUNGO ATIA NENO

Kwa upande wa Kocha wa  viungo wa timu hiyo(ftnes coach), raia wa Afrika ya kusini, Riedoh Berdien, alisema  kazi kubwa aliyo nayo ni kuhakikisha kila mchezaji anakuwa na misuli imara, ila kuzuia majeruhi ya mara kwa mara.

“Nimekuja kufanya kazi na Yanga nitahakikisha nawapigania wachezaji kuwa imara, na mazoezi  amabayo nawapa sio ya kawaida, lengo ni kuisadia timu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hatuweza kufanikiwa kama makocha  hatutafanya juhudi,”alisema Berdien.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here