Home Habari Kocha Simba ala bata Ubelgiji

Kocha Simba ala bata Ubelgiji

447
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU

KOCHA mkuu wa Simba, Patrick Aussems, kwasasa yupo nchini kwao Ubelgiji kwa mapumziko akijiweka sawa kwa msimu mpya wa 2019/20 ambapo kwa mara nyingine tena, Simba itaiwakilisha nchi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aussems aliandika katika mtandao wa wake wa Twitter ‘Back home… so happy to be with my beloved dog’ akimaanisha yupo nyumbani na anafuraha kubwa kukutana na na mbwa wake anayempenda huku akiweka picha akiwa ametulia na mbwa wake huyo.

Kocha huyo wa Simba amekuwa na msimu mzuri akiongoza Wekundu wa Msimbazi kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara wakiwazidi watani zao Yanga kwa pointi saba.

Aidha, Aussems aliipeleka Simba katika hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika na kukidhi masharti aliyowekewa na viongozi wake.

Uongozi wa Simba ulimuongezea mkataba wa mwaka moja kocha huyo raia wa Ubelgiji ambaye ameshaanza kukisuka upya kikosi chake kabla ya maandalizi ya msimu mpya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here