Home Michezo Afrika KOCHA WA ALGERIA ABWAGA MANYANGA

KOCHA WA ALGERIA ABWAGA MANYANGA

303
0
SHARE
Georges Leekens

FRANCEVILLE, Gabon

KOCHA wa Algeria raia wa Ubeligiji, Georges Leekens ametangaza kuachana na timu hiyo baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Afcon mwaka huu.

Algeria ilikuwa ni moja ya timu bora ambazo zilipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri lakini imeshindwa kufurukjuta kutokana na ushindani uliokuwepo msimu huu tofauti na misimu mingine.

Kwa mijibu wa taarifa yake kwa vyombo vya habari, Leekens amesema ameamua kuachana na timu hiyo ili kutafuta changamoto mpya hasa baada ya kushindwa kufikia malengo yake kama kocha ambayo yalikuwa ni kuifikisha Algeria fainali au nusu fainali ya Afcon.

“Nimeshindwa kufikia malengo niliyokuwa nimeyatarajia, kwa sababu hiyo sina namna ila ni kuwaachia watu wengine waweze kuendeleza timu hii wakichukua pale nilioishia mimi.

“Vile vile nahitaji kupata changamoto mpya kama mwanadamu mwenye malengo yangu, sababu hizi na nyingine ambazo siwezi kuzitoa hapa, naamua kuachaana na Algeria nikiwa na furaha na mwenye matumaini mapya, ninawatakia kila la kheri.

“Nimeshazungumza na wachezaji, nimewaeleza dhamira yangu vile vile niwameshawaambia waajiri wangu ambao ni Shirikisho la Soka Algeria juu ya kile nilichoamua na wamenikubalia na kunitakia kila la kheri,” amesema Leekens katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Algeria ilipangwa Kundi, B ambapo katika mechi tatu ilizocheza haijashinda zaidi ya kupata sare mbili na kufungwa mchezo mmoja.

Mchezo ambao timu hiyo ilifungwa ilikuwa ni dhidi ya Tunisia ambapo ilifungwa mabao 2-0 kisha kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Zimbabwe na idadi kama hiyo dhidi ya Senegal hivyo kutupwa nje ya michuano hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here