SHARE

NA GLORY MLAY


TIMU ya Taifa ya Kriketi ya vijana chini ya miaka 17, inatarajiwa kushuka dimbani leo dhidi ya Nigeria katika mchezo wa fainali ya michuano ya kufuzu Kombe la Dunia, utakaochezwa kwenye Uwanja wa Witrand, Afrika Kusini.

Michuano hiyo inayofikia tamati leo, ilikuwa  inashirikisha timu kutoka Tanzania, Sierra Leone, Msumbiji, Rwanda, Ethiopia, Ghana, Swaziland, Bostwana, Lesotho, Nigeria na wenyeji Afrika Kusini.

Mchezo wa kwanza walishinda dhidi ya Swaziland kwa mikimbio 262-99, wa pili ikashinda dhidi ya Rwanda kwa mikimbio 134-114, mchezo wa tatu ikaichapa Bostwana mikimbio 161-136 na mchezo wa nne dhidi ya Nigeria mikimbio 137-121.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Kocha wa timu hiyo, Peshotan Mehta, alisema wamefanya maandalizi ya kutosha, hivyo wanaamini wataifunga Nigeria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here