Home Michezo Kimataifa KUMBE ‘BABU’ FERGUSON ANAMPA MOURINHO SIRI ZA USHINDI MAN UNITED

KUMBE ‘BABU’ FERGUSON ANAMPA MOURINHO SIRI ZA USHINDI MAN UNITED

610
0
SHARE

MANCHESTER, England

KAMA ulikuwa unajiuliza na unakosa majibu juu ya nini kimeibadilisha Manchester United haraka hadi kuwa inatoa vichapo mfululizo, Mreno Jose Mourinho ameamua kufunguka na kuweka kila kitu hadharani.

Mourinho amefichua kuwa Sir Alex Ferguson amekuwa akitembelea mara kwa mara kwenye mazoezi ya Manchester United katika viwanja vya Carrington.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ferguson (74) kutembelea kwenye mazoezi ya United tangu alipostaafu kuifundisha timu hiyo mwaka 2013 na kupewa cheo cha Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo.

Ferguson ambaye amedumu United kwa miaka 26, alikuwa akifuatilia mechi tu za United na kutojihusisha na jambo lolote la kiufundi kwa takribani miaka mitatu sasa.

Lakini Mourinho aligundua kuwa anamhitaji zaidi mkongwe huyo kwenye mipango yake hivyo kumwalika kwenye mazoezi na kumpa muda wa kuzungumza na wachezaji juu ya historia ya klabu hiyo.

Akizungumza na mtandao wa United, Mourinho alisema: “Hakuwahi kufika hapa tangu alipostaafu lakini nimeamua kumrudisha ili aungane tena na watu wake.

“Nilitaka wachezaji waone watu wakubwa waliotengeneza historia ya klabu hii, kuzungumza nao na kula nao chakula pamoja. Kila mtu ana furaha na ujio wake.

“Mimi si mbinafsi. Naheshimu historia ya hapa na ninajua pia kuwa Ferguson anaipenda sana Manchester United. Tunazungumza kila siku na huwa namwambia kuwa hii ni nyumba yake.

Mourinho anaamini Ferguson alihusika kwa kiasi kikubwa mpaka yeye akapewa kazi na uongozi wa klabu hiyo japo alikiri hakuzungumza lolote na David Moyes, wakati United ilipoichapa Sunderland bao 3-1.

“Sizungumzi na kila mtu,” aliongeza Mourinho. “David ni mmoja wa watu ambao sikuzungumza naye lolote. Nafikiri unapokuwa kocha wa Manchester United unatakiwa utambue kuwa upo kwenye klabu kubwa duniani, hivyo hutakiwi kuwa na mawazo ya kawaida.

“Lakini kama unakuwa haupo na Manchester, huna timu au huna kazi ya kufanya, sidhani kama unakuwa kwenye matatizo makubwa. Nilifikiri kabla ya kuamua kuwa hapa na nilijiuliza pia kwanini United haikuwa na matokeo mazuri katika kipindi cha miaka mitatu.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here