Home Burudani KUMBE KAKOLANYA MTAMU KWA UPISHI AISEE

KUMBE KAKOLANYA MTAMU KWA UPISHI AISEE

7325
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE

LEO katika nje ya soka, tunaye mezani kipa wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Beno Kakolanya ambaye kwa sasa ni gumzo kubwa midomoni mwa mashabiki wa soka nchini.

Nini kimemfanya kuwa gumzo? Hakuna kingine zaidi ya ubora wake langoni alioanza nao msimu huu wa Ligi Kuu akiwa amecheza mechi sita mpaka sasa na kuruhusu wavu wake kutikiswa bao moja tu.

Kakolanya kipa wa zamani wa Tanzania Prisons, amekuwa kwenye ubora wa hali ya juu mbele ya mashabiki wa soka nchini kiasi cha kumfanya kocha wa Stars, Emmanuel Amunike, kutumia sekunde chache kumjumuisha katika kikosi chake.

DIMBA limepiga stori na Kakolanya kujua maisha yake nje ya soka ambayo wengi hawayafamu na hiki ndicho alichokieleza.

DIMBA: Unaishi wapi?

KAKOLANYA: Mabibo na familia yangu.

DIMBA: Unapenda kula chakula gani?

KAKOLANYA: Ndizi, ugali na wali.

DIMBA: Unajua kupika chakula chochote?

KOKOLANYA: Mimi ni mpishi mzuri wa ugali, ndizi, wali na pilau.

DIMBA: Kipato chako unachoingiza kutokana na kazi yako unakitumia kwenye matumizi gani?

KAKOLANYA: Mara nyingi huwa namtumia mama yangu na nyingine kwa ajili ya matumizi ya familia yangu na mimi mwenyewe.

DIMBA: Vitu gani lazima uwe navyo kabla ya kutoka ‘out’?

KAKOLANYA: Mara nyingi mimi sitoki out, napenda kukaa zaidi nyumbani na familia yangu.

DIMBA: Nguo gani ambazo hupendi kuvaa?

KAKOLANYA: Nguo fupi na zinazobana sana.

DIMBA: Kwenye soka unapenda kuvaa mavazi ya kampuni gani?

KAKOLANYA: Nike

DIMBA: Unapenda kukaa na washkaji wa aina gani?

KAKOLANYA: Mimi huwa napenda kuzungumza na kila rafiki huwa sichagui maana hujui ya kesho.

DIMBA: Stori gani ambazo zinakuboa ukiwa na marafiki zako mnazungumza?

KAKOLANYA: Za kuteta watu.

DIMBA: Kitu gani huwezi sahau tangu mwaka huu uanze?

KAKOLANYA: Majeraha ambayo yalinisababishia nikae nje ya uwanja kwa muda mrefu.

DIMBA: Kama ukisafiri kwenda nje ya nchi, utamiss vitu gani kutoka nyumbani?

KAKOLANYA: Huwa namkumbuka sana mama, mke, ndugu zangu na vyakula vya kwetu.

DIMBA: Unapenda starehe gani?

KAKOLANYA: Kuangalia movie.

DIMBA: Unapenda kuendesha gari ya aina gani?

KAKOLANYA: Mimi naendesha gari ya aina yoyote.

DIMBA: Maswali gani ambayo hupendi kuulizwa.

KAKOLANYA: Maswali magumu.

DIMBA: Kama usingecheza soka, ungefanya kazi gani?

KAKOLANYA: Mfanyabiashara.

DIMBA: Kitu gani ambacho kimekuwa ni changamoto kubwa mtaani kwako na kimekuwa kero kubwa kutokana na jina lako?

KAKOLANYA: Mtu kukujaji tofauti na wewe ulivyo wakati hakujui vizuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here