Home Michezo Kimataifa KUMBE PSG WALISHAPANGA MATOKEO NJE YA UWANJA

KUMBE PSG WALISHAPANGA MATOKEO NJE YA UWANJA

424
0
SHARE

PARIS, Ufaransa

KUMBE nyota wanne wa PSG walishaingiwa na mchecheto na Barcelona, hata kabla hawajakanyaga nyasi za Dimba la Nou Camp.

Habari hii imekuja baada ya kuvuja kwa video ikiwaonyoshe nyota wanne wa klabu hiyo, Marco Verratti, Blaise Matuidi, Thomas Meunier na Julian Draxler, wakizungumza hofu yao kwa Barca.

Video hiyo iliyorekodiwa kwenye ndege wakati PSG wakisafiri kuelekea nchini Hispania kwa ajili ya mchezo wa marudiano, nyota hao walijadili namna Barca walivyoweza kupindua matokeo kwenye mechi zilizopita.

“Dakika 20 za mwanzo tutakuwa kwenye hali ngumu sana,” alisema Matuidi. “Uwanja ni mkubwa sana ule. Ni lazima kila Neymar anapopata mpira, tunamfikia kwa haraka na kumpokonya.”

Ghafla Draxler, akadakia: “Msimu uliopita nikiwa na Wolfsburg, tulishinda mchezo wa kwanza dhidi ya Real Madrid, bao 2-0. Lakini baada ya dakika 20 pale Bernabeu, tulishalala 2-0 kabla ya Ronaldo kupachika bao la tatu dakika ya 80.”

Akaongeza: “Nafikiri tuliingia kwa hofu sana, maana hatukufanya shambulizi lolote la maana langoni mwao.”

Akitoa mfano mwingine wa kilichowakuta PSG, mbele ya Chelsea, Matuidi alisema: “Ilikuwa hivyo pia tulipocheza dhidi ya Chelsea. Tulishinda bao 3-0 nyumbani na kila mmoja akaamini kuwa kazi imeshamalizika. Lakini tulitua London kwa hofu kubwa na mwisho wa siku, tulichapwa bao 2-0 na kutolewa.”

Hofu hii ya wachezaji wa PSG, ikawatafuna kwenye mchezo dhidi ya Barca, walipolala bao 6-1 na kuibua hasira kwa mashabiki wao waliotishia kuwafanyia fujo walipotua kwenye uwanja wa ndege, Paris.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here