Home Michezo Kimataifa KUMBE WENGINE WALIJIPANGA KUIPIKU PSG KWA MBAPPE

KUMBE WENGINE WALIJIPANGA KUIPIKU PSG KWA MBAPPE

478
0
SHARE

PARIS, Ufaransa
RAIS wa klabu ya PSG, Nasser al-Khelaifi, amesema wao wana bahati sana kumnasa Kylian Mbappe, kwani kuna timu zilijipanga kutoa pesa nyingi zaidi ya watakazotoa wao baada ya msimu huu.
Mbappe anatarajiwa kuwa mchezaji wa pili ghali wa muda wote msimu ujao, baada ya kuwasili Paris mwaka huu kwa mkopo akitokea katika klabu ya Monaco.
Inakumbukwa kuwa, Mbappe aliwahi kuelezea namna gani alivyotamani kuichezea PSG, ambayo ilimnasa Neymar kwa bei ya rekodi, pauni milioni 199, lakini baada ya msimu huu kumalizika PSG watailipa Monaco pauni milioni 166 kwa ajili ya kinda huyo.
Klabu zilizokuwa zikimfukuzia Mbappe, ukiitoa PSG ni Arsenal, Manchester City na Real Madrid.
“Kwa kweli tulipata changamoto, kila klabu kubwa ilimtaka Mbappe. Kila klabu ilijipanga kutoa dau nono zaidi yetu, lakini tulimwelezea mipango yetu na nini tunachokihitaji siku za usoni, ukizingatia ni Mfaransa, ni mtu wa Paris na anaipenda hii klabu,” alisema al-Khelaifi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here