Home Michezo Kimataifa KUMSAJILI MCHEZAJI EVERTON UJIPANGE

KUMSAJILI MCHEZAJI EVERTON UJIPANGE

447
0
SHARE

MWANDISHI WETU NA MITANDAO

HIZI ni thamani za wachezaji wa Everton walioanza kipindi cha kwanza katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia.

Kikosi cha kwanza kilianza na mastaa kadhaa wakubwa, huku kukiwa na mchanganyiko wa vijana.

Ukiambiwa walianza mastaa si jina tu na ukisikia vijana usidhani ni wa bei chee. Thamani zao ziko juu kweli kweli.

Unaambiwa hata kinda ambaye alifunga bao la pili jana, thamani yake unawapata Obrey Chirwa wawili na Emanuel Okwi mmoja!

Nisikuchoshe, tiririka nao mwenyewe…

 

Everton ‘A’

Marten Stekelenburg- Mlinda mlango huyo aliyewahi kuzichezea timu za Roma, Fulham, Southampton, thamani yake ni pauni milioni 1.7 (shilingi bilioni tano za Kitanzania).

Ashley Williams- Beki huyo wa kati wa zamani wa Swansea, thamani yake ni pauni milioni saba (shilingi bilioni 20 za Kitanzania).

Phill Jagielka- Nahodha huyo wa Everton ambaye alidhihirisha uongozi wake dhidi ya wachezaji wa Gor Mahia, ana thamani ya pauni milioni 1.7 (shilingi bilioni tano za Kitanzania).

Calum Connoll- Beki huyo kinda aliyeanza upande wa kushoto juzi, ni zao la akademi ya klabu ya Everton ambaye ametumia miaka miwili kucheza timu za vijana na kutolewa kwa mkopo timu za Wigan na Barnsley. Thamani yake haijatajwa.

Jonjoe Kenny- Kinda huyo naye alianza kama beki wa kulia juzi. Naye ni zao za akademi ya Everton. Thamani yake haijatajwa.

Morgan Schneiderlin- Moja ya wachezaji waliokuwa vivutio katika mchezo wa juzi. Kiungo huyo wa zamani wa Southampton na Man United, ana thamani ya pauni milioni 19 (shilingi bilioni 55.6 za Kitanzania).

James McCarthy- Kiungo huyo aliyewahi kuitumikia Wigan, ana thamani ya pauni milioni 13 (shilingi bilioni 37.9 za Kitanzania).

Davy Klaassen- Kiungo mchezeshaji huyo wa Kidachi ametua Everton mwaka huu akitokea Ajax ya Uholanzi, thamani yake sokoni ni pauni milioni 15.8 (shilingi bilioni 45.5 za Kitanzania).

Aaron Lennon-Kwa sasa anaonekana kupungua makali lakini wadau wa soka hawawezi kumsahau winga ‘teleza’ huyo wa zamani wa Spurs mwenye thamani ya pauni milioni nne (shilingi bilioni 12.6 za Kitanzania).

Ademola Lookman- Kinda huyo raia wa England mwenye asili ya Nigeria, ndiye aliyetoa pasi ya bao la Rooney, thamani yake sokoni ni pauni milioni nne (shilingi bilioni 12.6 za Kitanzania).

Wayne Rooney- Mfungaji wa bao la kwanza kwa Everton juzi. Straika huyo ana thamani ya pauni milioni 13 (shilingi bilioni 37.9 za Kitanzania).

 

Everton ‘B’

Baada ya kuzifahamu thamani za nyota wa Everton walioanza kipindi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Gor Mahia, hii sasa ni orodha ya wale wa kikosi cha pili ambao kwa maoni ya wadau wengi wa soka walioshuhudia mchezo huo, walisema kuwa ndio walioonesha soka maridadi mno.

Mateusz Hewelt- Kipa huyo kinda aliyeanza kipindi cha pili juzi, ni mojawapo ya zao la akademi ya Everton, thamani yake haijatajwa.

Michael Keane- Beki huyo wa kati alisajiliwa na Everton wiki chache zilizopita akitokea Burnley, thamani yake ni pauni milioni 13.5 (shilingi bilioni 38.6 za Kitanzania).

Muhamed Besic- Huyo ni kiungo mkabaji ambaye kutokana na uwezo wake wa kukaba, juzi akaanzishwa kipindi cha pili kama beki wa kati, thamani yake ni pauni milioni 3.7 (shilingi bilioni 10.7 za Kitanzania).

Mathew Pennington- Beki huyo wa kulia zao la akademi ya Everton, ana thamani ya pauni 375,239 sokoni (shilingi bilioni moja za Kitanzania).

Leighton Baines- Beki huyo wa kushoto aliyedumu na Everton kwa muda wa miaka 10, ana thamani ya pauni milioni 5.6 (shilingi bilioni 16 za Kitanzania).

Idrissa Gana Gueye- Kiungo mkabaji huyo anayekubalika na wadau wa soka, thamani yake sokoni ni pauni milioni 13.7 (shilingi bilioni 39 za Kitanzania).

Gareth Barry- Mkongwe huyo wa soka England anayefukuzana na watu kama Ryan Giggs kwenye wingi wa mechi za EPL, ana thamani ya pauni milioni moja (shilingi bilioni tatu za Kitanzania).

Tom Davies- Kiungo huyo ambaye pia ni zao la akademi ya soka ya Everton, ana thamani ya pauni milioni sita (shilingi bilioni 17 za Kitanzania).

Kieran Dowell – Mfungaji huyo wa bao kali la ushindi la Everton juzi, ana thamani ya pauni 188,061 (shilingi milioni 538.7 za Kitanzania).

Kevin Mirallas- Winga huyo aliyewahi kuzichezea Lille na Olympiacos, ana thamani ya pauni milioni 9.7 (shilingi bilioni 27.9 za Kitanzania).

  1. Calvert-Lewin- Huyo ni shujaa wa timu ya taifa ya England U20 iliyotwaa Kombe la Dunia la vijana baada ya kufunga bao pekee la ushindi dhidi ya Venezuela. Thamani yake sokoni ni pauni milioni 2.6 (shilingi bilioni 7.5 za Kitanzania).

Vikosi hivyo viwili vilikuwa na mastaa sita wenye thamani kubwa zaidi kuliko wenzao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here