Home Habari KWASI ATULIZA MZUKA MASHABIKI

KWASI ATULIZA MZUKA MASHABIKI

6810
0
SHARE

NA TIMA SIKILO


BEKI wa kushoto wa Simba, Asante Kwasi, amewaambia mashabiki wa timu hiyo wasiwe na hofu kuhusu afya yake kwani anaendelea vizuri na muda wowote atarudi dimbani.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Kwasi alisema hali yake haikuwa nzuri sana kwa muda wa wiki moja kutokana na maradhi ya tumbo yaliyokuwa yakimsumbua lakini kwa sasa hali si mbaya na anaendelea na matibabu.

Alisema kutokuwepo kwake hakuwezi kuacha pengo katika kikosi chao kwani wachezaji wote waliopo wako vizuri na anaamini wanaweza kupata matokeo ya kufurahisha.

“Naendelea vizuri japo nipo kwenye matibabu najua muda si mrefu nitakuwa sawa na kuanza mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa, kutokuwepo kwangu kikosini hakuwezi kuathiri kitu chochote kwani kikosi chetu chote kina wachezaji wazuri,” alisema Kwasi Asante.

Akizungumzia mbio za kutetea ubingwa wao, Kwasi alisema kutokana na namna kikosi chao kilivyo anatarajia kwamba malengo yao yatatimia.

Alisema wanachohitaji ni kuhakikisha wanatetea ubingwa wao lakini pia kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa ambayo Simba wataiwakilisha nchi katika michuano ya  Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here