SHARE

 

Paul PogbaMICHUANO ya Euro inaendelea kushika kasi nchini Ufaransa ambapo mpaka sasa mataifa yote 24 yameshacheza mechi zao za kwanza za makundi.

Wenyeji wa michuano hii, timu ya Ufaransa itashuka tena dimbani usiku wa leo kupambana na Albania, baada ya mchezo wa kwanza kufanikiwa kupata ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Romania.

Kwenye ushindi huo wa mabao ya Olivier Giroud na kiungo wa West ham, Dimitri Payet, Ufaransa walionekana kuzidiwa kimbinu na Romania.

Kijiweni wiki hii tunakuletea moja ya mjadala mkubwa ulioibuka kwenye vibanda umiza wakati mashabiki wakilifuatilia pambano la Ufaransa dhidi ya Romania.

Utata ulikuwa ni juu ya Paul Pogba. Ni kweli kiwango chake kinafanana na thamani na ubora unaoandikwa kwenye magazeti?

Kiungo huyu wa klabu ya Juventus amekuwa akitajwa kuwa na kiwango kikubwa na mchezaji mwenye thamani sana kutoka Ligi Kuu Italia, Seria A.

Hivi sasa katika dirisha la usajili, Pogba anatajwa kugombewa na klabu za Real Madrid na Manchester United aliyowahi kuichezea kabla ya kwenda Juventus.

Taarifa zinasema kuwa Madrid na United wako tayari kulipa kiasi cha pauni milioni 75 kwa ajili ya Pogba. Kweli jamani Pogba ana thamani hii?

Nisimalize maneno, uwanja ni wako msomaji wetu mpendwa wa safu hii kutuambia mtazamo wako katika hili, ni kweli Pogba ana thamani sawa na kiwango chake?

 

Matokeo wiki iliyopita

WIKI iliyopita kwenye safu hii pendwa ya kijiwe utata tuliweka mjadala wa kuangalia kama timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inapaswa kuletewa kocha wa kigeni au iendelee kukomaa tu na kocha mzawa?

Mjadala huu ulikuja kufuatia matokeo mabovu yanayoikabili timu hii kwenye michuano mbalimbali inayoshiriki.

Katika meseji nyingi zilizotumwa na wasomaji wetu, zilipendekeza ni bora TFF itafute kocha wa kigeni wa kuja kumsaidia kocha mzawa wa sasa, Charles Boniface Mkwasa.

Pamoja na kushindwa kwa Samatta kuitetea Stars kwa kukosa penalty, lakini bado anabaki kuwa ni mchezaji bora Tanzania. 0752592029

Mkwasa hakustahili kuwa kocha mkuu kwa sababu ya Usimba na Uyanga, hivyo apatiwe kocha wa kigeni na yeye abaki kuwa msaidizi wake. 0626573372

Naitwa Maulid Hassan wa Mbagala wa Dar es Salaam, mtazamo wangu wabaki hao hao kwa sababu tunagawana machungu timu ikifungwa, suala la maendeleo ni kujipanga tu na kuwekeza kwa vijana na kuondoa Usimba na Uyanga. 0653542293

Naitwa Uwesu wa Dodoma, Taifa Stars iletewe kocha wa kigeni mwenye uwezo kama wa Pluijim au zaidi. 0716548628

Taifa Stars iletewe kocha wa kigeni, Mkwasa hafai kwani hajawahi hata kuipandisha timu yoyote daraja na hata timu ya wanawake ilimshinda akajiuzulu hana uwezo mimi mzee Sonyo wa Kagera, Dar es Salaam. 0653 667864

Mimi nadhani kuna haja ya kuleta makocha wa kigeni kwa wazawa bado sana Iccra Ponela wa Mikese Morogoro. 0713955618

Naitwa Sikunjema wa Chamazi, kocha wa kigeni ni muhimu ila kwa timu ile hata angekuwa Wenger tungefungwa kwa sababu idadi ya wachezaji wanaocheza nje ya nchi wenye ubora ni wawili tu, tatizo wachezaji wa Tanzania hawapendi kucheza nje. 0713473550

Ili kuepuka kuchaguliwa mateja, kocha wa kigeni ni muhimu kwa timu ya Taifa. 0752350778

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here