SHARE

LONDON, ENGLAND

KOCHA mkuu wa klabu ya Chelsea, Frank Lampard, ameonyesha wazi hataki masikhara hata kidogo na hiyo imedhihirika mara baada ya mkufunzi huyo kumuonyesha mlango wa kutokea beki David Luiz ambaye ametua Arsenal.

Jumatano asubuhi kocha huyo aliweka wazi hamhitaji katika kikosi chake beki huyo ambaye walitwaa pamoja taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2012.

Licha ya kukabiliwa na mechi ngumu dhidi ya Manchester United, Lampard hajasita kuachana na beki huyo ambapo sasa amepanga kuwatumia vijana Andreas Christensen na Kurt Zouma katika mchezo huo huku Antonio Rudiger na Fikayo Tomori wakisubiri benchi.

 “Siku ambayo David hakufanya mazoezi ni maamuzi yangu. Kamwe huwa sishangazwi na wachezaji. Kuna tofauti kubwa kati ya kuwa mchezaji na kocha unapokuwa mchezaji unakuwa mbinafsi wala hujali kuhusu wengine, lakini unapokuwa kocha jukumu lako ni la watu 25, nachukia kuangushwa na ninahofia,” alisema Lampard.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here