Home Michezo Kimataifa LAMPARD: MOURINHO ATABAKI KUWA ‘THE SPECIAL ONE’

LAMPARD: MOURINHO ATABAKI KUWA ‘THE SPECIAL ONE’

5962
0
SHARE

MANCHESTER, England


KOCHA wa Derby County, Frank Lampard, anaamini bado kocha wa Manchester United ni ‘The Special One’ tofauti na anavyochukuliwa kuwa ameishiwa mbinu kwa sasa baada ya kutokuwa na mwendelezo mzuri wa ligi.

Jumamosi iliyopita Mourinho alijikuta anaambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Wolves, mchezo uliopigwa dimba la Old Trafford na kumfanya kukosolewa mbinu zake na mchezaji wa bei ghali, Paul Pogba.

Lakini imekuwa tofauti kwa mchezaji wa zamani wa Chelsea, Lampard, ambaye anasema hajawahi kuwa na shaka na uwezo wa Mourinho akiamini bado ni kocha imara kusimamia anachokiamini.

“Kwangu anabaki kuwa ‘The Special One’ kwa makocha wote duniani, ni mtu ambaye hayumbishwi, Tottenham wana kocha mkubwa kama ilivyo kwa Liverpool,” alisema.

Usiku wa jana Lampard alikiongoza kikosi chake hicho kinachoriki Ligi Daraja la Kwanza (Championship) dhidi ya Man United, mchezo wa Kombe la Carabao uliopigwa Uwanja wa Old Trafford.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here