SHARE

TOKYO, Japan

KOCHA mpya wa Chelsea, Frank Lampard amesema kwamba kazi yake ya kuinoa timu hiyo ataifanya kwa njia zake na hatotegemea ushauri kutoka kwa makocha wa zamani waliopita hapo.

Hata hivyo, kocha wa zamani wa Chelsea, Guus Hiddink ameripotiwa kuwasiliana na Lampard takribani wiki mbili zilizopita ingawa hawakuzungumza kwa urefu, lakini hakuna mawasiliano kati yake na Jose Mourinho au Carlo Ancelotti.

Kwa sasa Lampard anakabiliwa na jukumu la kuiongoza timu hiyo ikiwa inatumikia adhabu ya kutosajili, kitu ambacho makocha waliopita Chelsea hawakuwahi kukutana nacho.

“Siwezi kuzungumza nao kwa sababu hali iliyopo sasa ni tofauti na waliyokutana nao wao. Hivyo, siwezi nikawaomba ushairi. Nieleweke, huwa ninawasiliana na Mourinho na hata Ancelotti. Hiddink pia.

“Ninawaheshimu, lakini nitajaribu kujifunza kupitia mimi, kupitia muda wote ambao nitakuwa na wachezaji wangu. Kama nitakuwa na haja ya kuwatafuta, nitawatafuta,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here