SHARE

JESSCA NANGAWE

WAKATI wachezaji mbalimbali wakiwa kwenye mapumziko kufuatia janga la virusi vya Corona, beki wa Simba, Erasto Nyoni, amesisitiza atatumia vizuri kipindi hiki kusimamia maelekezo ya daktari ili kurudi kwenye afya yake.

Nyoni ambaye aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, alitakiwa kukaa nje kwa takribani wiki mbili kabla ya kuanza mazoezi mepesi.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, beki huyo alisema pamoja na ligi kusimama lakini muda mwingi amekuwa akizingatia maelekezo ya daktari ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi mepesi akiamini atakaa sawa baada ya siku 30.

“Kwa sasa naendelea vizuri, pamoja na ligi kusimama lakini natumia muda mwingi kufuata maelekezo ya daktari ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi mepesi, cha msingi natamani kurejea uwanjani baada ya ligi kurejeshwa rasmi,” alisema Nyoni.

Aidha Nyoni anaamini ligi hiyo itaendeleza makali yake kama awali licha ya mapumziko hayo, huku akisisitiza kuwa Simba wataweka rekodi nzuri sambamba na kutwaa ubingwa huo msimu huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here