Home Habari LINAH: NIMERUDI UPYA KAENI TAYARI KUNIPOKEA

LINAH: NIMERUDI UPYA KAENI TAYARI KUNIPOKEA

694
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa kizazi kipya, Linah Sanga, amesema mara baada ya kutoka kwenye likizo ya uzazi sasa anarudi sokoni kivingine kwa kuhakikisha anarudisha heshima ya jina lake.

Linah, ambaye alijifungua hivi karibuni, amesema muda wa kukaa na mwanawe karibu zaidi umetosha, kwa kuwa sasa anaweza kumwacha nyumbani na kuendelea na shughuli zake za muziki.

“Mashabiki wangu wategemee wimbo mpya mwezi huu wa 12 mwishoni, nimefanya kolabo na Recho yule wa wimbo wa ‘Kizunguzungu’, nafikiri wiki ijayo tutaachia,” alisema Linah.

Hii inakuwa kolabo ya pili kwa Linah akimshirikisha Recho, baada ya wawili hao kukutana katika ngoma moja baada ya kushirikishwa na kundi la Makomando katika ngoma yao inayokwenda kwa jina la Chap Chap.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here