SHARE

MERSEYSIDE, England

HII sasa sifa! hao Liverpool hawawezi kukuelewa kama utawaambia waache kufanya usajili wa straika wa Napoli, Lorenzo Insigne, ambaye aliifanya timu hiyo kutoka nchini England kuishi maisha magumu Italia kwa kufunga bao dakika za mwisho katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kutokana na Mohamed Salah kushindwa kuwa na makali kama msimu uliopita, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amepeleka jina la Insigne kwa vigogo wa timu hiyo waanze kulifanyia kazi mapema kabla wengine hawajaingiza miguu.

Hivi karibuni timu ya Chelsea ilitajwa kumwania straika huyo ambaye aliwahi kufundishwa kwa misimu minne na Maurizio Sarri wakati yupo Napoli.

Insigne, 27, mpaka sasa amefanikiwa kucheza michezo 360 akiwa na jezi ya Napoli na kufunga mabao 116 lakini tangu kuanza kwa msimu huu amepachika mabao nane.

Lakini kiwango cha Salah na Roberto Firmino kimekuwa kikiwapa hofu mashabiki na benchi la ufundi la Liverpool tangu kuanza kwa msimu wakionekana kucheza chini ya kiwango.

Kama wakifanikiwa kupata saini ya Insigne itawapa nyongeza kubwa katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ambayo tangu kuanza kwa msimu huu, Sadio Mane amekuwa kwenye kiwango cha juu.

Inadaiwa kuwa Liverpool wapo tayari kutoa dau la pauni milioni 72 kumvuta straika huyo raia wa Italia na kama ikishindikana, wapo tayari kumjumuisha na Dominic Solanke kwenye dili hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here