Home Michezo Kimataifa LOOKMAN AZIGONGANISHA NIGERIA NA ENGLAND

LOOKMAN AZIGONGANISHA NIGERIA NA ENGLAND

405
0
SHARE
Ademola Lookman

LONDON, England

UNAZIKUMBUKA zile bao 4-0 alizopigwa Man City na Everton pale Goodison Park? Mabao mawili kati ya manne yalifungwa na makinda wawili, mmoja Mzungu mwingine Mwafrika, jina lake ni Ademola Lookman.

Lookman ana umri wa miaka 19, mzaliwa wa London, England mwenye asili ya Nigeria, ameamsha vita baina ya mataifa hayo mawili ambayo yanamgombania fowadi huyo aliyeonesha kiwango kizuri tangu atue Everton kwa dau la pauni milioni 11, Januari mwaka huu.

Nigeria wameonesha nia ya dhati ya kumnyakua kinda huyo, ambapo wawakilishi wake walikaa meza moja na Chama cha Soka Nigeria kwa mazungumzo juu ya hatima yake ya soka la kimataifa huku pia akiwahi kuiwakilisha England kwenye timu za vijana chini ya miaka 19 na 20.

Katika kuonesha kwamba wana nia ya kweli ya kuwa na Lookman, kocha wa timu ya taifa ya Nigeria, Gernot Rohr, anataka kumtunzia nafasi kwenye kikosi kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Senegal mwezi ujao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here