SHARE

MILAN, ITALIA

NYOTA ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji, Romelu Lukaku imeanza kung’aa katika mchezo wa kwanza  wa Ligi Kuu ya Italia Serie mara baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 4-0 ilioshinda klabu ya Intermillan dhidi ya Lecce.

Makosa yaliyofanywa na mlinda mlango wa Lecce, Gabriel parried baada ya kuutema mpira uliopigwa na Lautaro Martinez ulimfanya staa huyo wa Ubelgiji afungue akaunti yake ya mabao Serie A.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 alianza kwa kishindo na kuwadhihirishia mashabiki  65,000 wa Inter waliojitokeza uwanjani  kuwa hajatua hapo kimakosa.

“Lukaku ameingia katika ulimwengu wa Inter katika njia nzuri lakini katika unyama wa aina yake.

“Ni kipande cha mwanaume chenye tabasamu, yupo tayari kufanya kazi pamoja na timu. Lakini sio Lukaku pekee aliyefanya vyema hata Lautaro alifanya vizuri,” alisema Conte.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here